XtGem Forum catalog

Kutamani kwako kwenda Mbinguni au kuyatamani mambo mazuri ya Mbinguni hakuwezi kukusaidia lolote ama kukufanya upone katika adhabu ile ya milele bali ni kufanya uamuzi kwa kujikana nafsi na ukiamua kumfuata Yesu mfuate kweli kweli ili usiwatumikie mabwana wawili. Ya duniani kweli yanapendeza lakini maandiko yanasema tusiviangalie vinavyoonekana bali tuviangalie visivyoonekana. Ni mara ngapi wewe umeisikia sauti ya Mungu nawe hutaki kuitika? Je wajua saa utakapokatishwa maisha yako aidha kwa ugonjwa, ajali au kwa kuuawa? Ndugu nakusihi umrudie Mungu wako maana itafika kipindi atazuia lolote utakalolihitaji kutoka kwake. Ila tumwombe Mungu na tukiamini kila tutakalomwomba litakuwa letu. Yanasema Maandiko katika Marko 11.24